tuwasiliane

Monday, December 19, 2016

Phiri achukizwa na Fanja kuchelewesha ITC ya Ngassa

Kinnah Phiri - Mbeya City

Kocha wa Mbeya City Mmalawi Kinnah Phiri,  ameilalamikia klabu ya Fanja ya Oman kwa kushindwa kutuma mapema kibali cha uhamisho ITC ya mchezaji Mrisho Ngassa ambaye alishindwa kuichezea timu yake dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi iliyopita.
Phiri amekiambia chanzo kimoja kuwa, kumkosa Ngassa kwenye mchezo huo ilikuwa pengo kubwa kutokana na kushindwa kushindwa kuzitumia vizuri nafasi nyingi walizotengeneza kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu hizo kutofungana.
“Ukweli nimeuambia uongozi uliandikie barua Shirikisho la soka FIFA, kulalamikia ucheweleshwaji wa ITC ya Ngassa kwasababu kama tumeweza kukamilisha taratibu zote za uhamisho kwanini wasiitume sasa mchezaji amekuwa akifanya mazoezi bila kucheza na sisi tunamtegemea,”amesema Phiri.Kocha huyo amesema katika mchezo huo waliweza kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi lakini tatizo lao lilikuwa kwenye umaliziaji, na hapo ndipo alipomkumbuka Ngassa.
Phiri amesema tangu mchezaji huyo ajiunge na timu yao amekuwa akifanya vizuri mazoezini jambo ambalo limempa matumaini ya kufanya vizuri na kuwa moja ya timu itakayopigania ubingwa wa ligi ya Vodacom msimu huu.
“Ujio wa Ngassa na mwenzake Zahoro Pazzi, kumenipa matumaini ya kufanya vizuri na kuwa moja kati ya timu nne zinazopigania ubingwa kwasababu hawa ni wachezaji wenye uzoefu na ligi hii na wameshawahi kucheza timu kubwa Tanzania,”amesema Phiri.
Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mbeya City, lakini juzi alishindwa kuitumikia timu hiyo kutokana na kutokuwa na Kibali cha Uhamisho wa Kimataifa (ITC), ambacho kimechelewa kufika kutokana na timu alikotoka, Fanja ya Oman kutokitoa kwa wakati.

No comments:

Post a Comment