tuwasiliane

Monday, December 19, 2016

Bruce Kangwa wa Azam aendelea kupeta Zimbabwe

Bruce Lange squeamish mpira na Kelvin Yondani kwenye pambano LA Ligi baina ya Azam na Yanga ( Picha ya Hisani)
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zimbabwe, Callisto Pasuwa amemjumuisha beki wa Azam, Bruce Kangwa katika kikosi chake cha awali kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazochezwa mwezi ujao nchini Gabon.

Pauwa anatarajiwa kukata majina na kubakia kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wataokaelekea Gabon kupeperusha bendera ya Zimbabwe katika fainali hizo zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 14.
Kangwa ambaye amekuwa akichezeshwa kama beki wa kushoto katika kikosi cha Azam alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu na amekuwa mmoja wa wachezaji wasiokosekana katika kikosi cha  kocha Mhispania, Zeben Hernandez.
Zimbabwe imepangwa katika kundi B la AFCON pamoja na Algeria, Tunisia na Senegal ikiwa mwakilishi pekee wa Kanda ya Kusini mwa Afrika.
Kikosi Kamili:
 Walinda Milango: Tatenda Mukuruva (Dynamos), Bernard Donovan (How Mine), Nelson Chadya (Ngezi Platinum Stars) na Takabva Mawaya (Hwange)
Walinzi: 
Lawrence Mhlanga, Teenage Hadebe (Chicken Inn), , Costa Nhamoinesu (Sparta Prague, Jamhuri ya Czech ), Onismor Bhasera (SuperSport United, Afrika Kusini), Blessing Moyo (Maritzburg United, Afrika Kusini), Tendai Ndlovu (Highlanders), Hardlife Zvirekwi (Caps United), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum Stars), Oscar Machapa (AS Vita, JK Kongo ) na Elisha Muroiwa (Dynamos)
Midfielders: 
Marvelous Nakamba (Vitesse, Uholanzi), Willard Katsande (Kaizer Chiefs, Afrika kUsini), Khama Billiat (Sundowns, Afrika Kusini), Knowledge Musona (K.V. Oostende, Ubelgiji), Danny Phiri, Kudakwashe Mahachi (Golden Arrows, Afrika Kusini), Raphael Kutinyu (Chicken Inn), Ronald Chitiyo (Harare City), Marshal Mudehwe (FC Platinum)  Talent Chawapiwa (ZPC Kariba) na Bruce Kangwa (Azam FC, Tanzania)
Strikers: 
Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang, China), Tendai Ndoro (Orlando Pirates, Afrika Kusini), Evans Rusike (Maritzburg, Afrika Kusini), Mathew Rusike (Helsinborg IF, Sweden), Cuthbert Malajila (Bidvest Wits, Afrika Kusini), na Tinotenda Kadewere (Djurgårdens IF, Sweden)

No comments:

Post a Comment