tuwasiliane

Wednesday, December 14, 2016

MBUYU TWITE,KUTUA MAJIMAJI

Mbuyu Twite
Kiungo mkabaji aliyemaliza mkataba wake katika klabu ya Yanga, Mbuyu Twite yuko mbioni kutua katika klabu ya Majimaji.
Twite anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja leo baada ya mazungumzo kati yake na  viongozi wa Majimaji kufikia pazuri.
Kocha wa Majimaji, Kally Ongala anamuhitaji Twite ili kuweza kumtumia katika kampeni  ya kuinusuru na janga la kushuka daraja katika ngwe ya lala salama inayotarajiwa kuanza Jumamosi.
Majimaji imepania kufanya kweli baada ya kumsajili mshambuliaji wa Stand United, Kelvin Sabato Kongwe pamoja na kipa raia kutoka Cameroun Antorien Toukam.Jitihada za blog hii kufanya mawasiliano na uongozi wa Majimaji ili kuweza kuzithibitisha taarifa hizi ziligonga mwamba,kwani simu zao zilikuwa zikiita tu bila kupokelewa

No comments:

Post a Comment