tuwasiliane

Wednesday, December 14, 2016

AME ALI ATUA KAGERA SUGAR KWA MKOPO

Ame ALI
Kiungo mshambuliaji wa Azam, Ame Ali aliyeichezea Simba kwa mkopo katika ngwe ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara ametua Kagera Sugar.
Ame Ali alisajiliwa na Azam akitokea Mtibwa Sugar lakini alishindwa kupata namba katika kikosi kilichokuwa chini ya kocha Stewart Hall.
Mwanzoni mwa msimu huu alitolewa kwa mkopo katika klabu ya Simba, hata hivyo alishindwa kupata nafasi ya kuonesha uwezo wake.
Katika klabu ya Kagera Sugar anaungana na kocha wake, Mecky Mexime aliyemfundisha kipindi akiwa Mtibwa Sugar msimu wa 2014/15 aliowika kiasi cha kuwavutia Azam.

No comments:

Post a Comment