tuwasiliane

Friday, December 2, 2016

DEAL DONE;YANGA YAMSAJILI JUSTINE ZULU KUTOKA ZESCO

Zulu katika mapambano yake
Kiungo mkabaji raia wa Zambia Justine Zulu amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga mabingwa watetezi wa taji la VPL na Azam Sports Federation Cup (FA Cup).
Kaimu Mkurugenzi wa Yanga Baraka Deusdedit amekiri kuwa mchezaji huyo ameshakamilisha michakato yote na amesaini mkataba kutua Jangwani, hata hivyo kiongozi huyo wa Yanga amekataa kuweka bayana muda wa mkataba alioingia mchezaji huyo lakini kwa mujibu wa taarifa amesaini miaka miwili.

Aidha, Deusdedit aliulizwa kuwa ni nani ataondoka Yanga kumpisha mchezaji huyo mpya lakini hakuweza kuelezea moja kwa moja, ingawa ametamka kuwa wapo wachezaji ambao wakimaliza mkataba wao hawatapewa nafasi tena.

Zulu alikua akiichezea Zesco United ya Zambia ambayo ilikuwa chini ya kocha wa sasa wa Yanga George Lwandamina ana miaka 27 huku akiwa na uzoefu unaotokana na kucheza soka la kulipwa nje ya Afrika pamoja na Afrika kwenye ligi zenye ushindani ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini.
Zulu amewahi kuzitumikaia klabu za National Assembly, Hapoel Be’er Sheva, Hapoel Bnei Lod, Hapoel Rishon LeZion, Enosis Neon Paralimni, Lamontville Golden Arrows, Kabwe Warriors na ZESCO United.

Mwaka 2012 alisaini miaka mitatu kuitumikia klabu ya Lamontville Golden Arrows ya Afrika Kusini. Oktoba 2013 alirejea kwenye ligi ya Zambia na kujiunga na  Kabwe Warriors, ukiwa ni mkataba wa muda mfupi. Baadaye alijiunga na Zesco United kuelekea msimu wa 2014 ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa.

Mwaka 2011 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Zambia. Zulu alikuwa sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012 lakini hakufanikiwa kutajwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 waliotwaa taji hilo mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment