tuwasiliane

Tuesday, December 13, 2016

Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya Ballon d'Or 2016

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa sasa wameshinda tuzo hii wakipokezana kwa miaka tisa mfululizo
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.
Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.
Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.Kwa sasa ameshinda Ballon d'Or 2008, 2013, 2014 na 2016 na tokea mwaka 2009 amekuwa akipokezana na Messi.
''sikuwahi kuwaza kama ningeshinda Ballon d'Or mara nne'' nina furaha kubwa sana, najisikia fahari'' alisema Ronaldo.
''Natumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji wenzangu, timu yangu ya taifa, makocha na watru wote walionisaidia kupata tuzo hii.''Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amefunga magoli 19 katika michezo 20 kwa klabu na timu ya taifa msimu huu.

Orodha ya wachezaji bora wa dunia tokea mwaka 2003

2016: Cristiano Ronaldo
2015: Lionel Messi
2014: Cristiano Ronaldo
2013: Cristiano Ronaldo
2012: Lionel Messi
2011: Lionel Messi
2010: Lionel Messi
2009: Lionel Messi
2008: Cristiano Ronaldo
2007: Kaka
2006: Fabio Cannavaro
2005: Ronaldinho
2004: Andriy Shevchenko
2003: Pavel Nedved

No comments:

Post a Comment