tuwasiliane

Thursday, November 17, 2016

Simba haitaki kurudia kosa, Yawapa mkataba Zimbwe na Mkude

Jonas Mkude wa Simba akishangilia 2016
Klabu ya Simba imeamua kuwaongezea mkataba wachezaji wake wawili Mohamed Hussein‘Zimbwe Jr’ na nahodha wake Jonas Mkude.
Katibu mkuu wa timu hiyo Patrick Kahemela amekiambia chanzo chetu, wamefikia maamuzi hayo baada ya kuona wapinzani wao Yanga wakiwanyatia nyota hao kwa ajili ya kuwasajili mara baada ya mikataba yao kumalizika.
“Tumeshafanya mazungumzo nao na siku mbili hizi tunatarajia kumalizana nao kwa kila mmoja wao kusaini mkataba mpya ya miaka miwili ili kuzima jaribio la Yanga kutaka kuwanyakua,” amesema Kahemela.
Katika huyo amesema mbali na nyota hao lakini pia wapo katika mchakato wa kuboresha maslahi na mikataba ya wachezaji wengine ambao wamebakiza muda mchache ili kumaliza muda wao wa kuichezea Simba.
Amesema wanachofanya kwasasa ni kuzungumza na kocha na kuangalia ni mchezaji gani wa zamani ambaye atakuwa anamuhitaji siku zijazo ili waweze kumuongezea mkataba wake aendelee kuichezea Simba.
“Tusingependa kurudia makosa ya kuacha mchezaji au kuchelewa kuwapa mikataba mipya wachezaji alafu wakachukuliwa na Yanga kama ilivyotokea huko nyuma ndiyo maana tupo makini hivi sasa kuhakikisha kila mchezaji ambaye anamchango kwenye timu yetu anaongezewa mkataba ili tuendelee kuwa naye,”amesema Kahemela.
Amesema wanafanya hivyo kwasababu wamegundua sababu ya kushindwa kufanya vizuri katika misimu minne iliyopita ni kushindwa kuwa karibu na wachezaji wao na kuwapa nafasi wapinzani wao kuwarubuni na kuwachukua
Hivi karibuni nahodha huyo amewahi kukaririwa na vyombo vya habari akitaka kuachana na Simba ili aweze kujiunga na Yanga kwa madai ya kucheweleshewa mshahara wake sambamba na wachezaji wenzake wa kikosi hicho ambacho kimemaliza mzunguko wa kwanza kikiwa kileleni mwa ligi ya Vodacom kwa kukusanya pointi 35 katika michezo 15 waliyocheza.

No comments:

Post a Comment