tuwasiliane

Saturday, November 19, 2016

Kauli ya Azam fc kuhusu Farid kuchelewa kwenda Hispania

Jafar Idd na Farid Musa wakiwa na nyuso za tabasamu baada ya kukutana kwa mara nyingine ikiwa ni muda mrefu umepita bila kuonana
Uongozi wa klabu ya Azam FC umeendelea kutoa ufafanuzi wa suala la kiungo mshambuliaji Farid Mussa Malik amabaye alifuzu kucheza soka nchini Hispania baada yta kupita katika majaribio ya klabu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili.
Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy amesema lengo lao kwa sasa ni kuhakikisha mchezaji huyo anaelekea barani Ulaya na kutimiza melngo ya kujiendeleza katika soka la ushindani, na si kuendelea kubaki hapa nchini kama inavyodhaniwa na walio wengi.
Amesema kinachoendelea kukwamisha mpango wa safari yake ya Hispania ni taraibu za upatikanaji wa kibali cha kufanyia kazi atakapofika nchini humo, hivyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano dhidi ya viongozi wa Deportivo Tenerife.
“Lengo la Azam ni kuona Farid anakwenda kucheza Tenerife kucheza mpira na si kurudi nyuma tena kucheza Azam FC kama wengine wanavyofikiria labda tunamkwamisha, kama tunamkwamisha tusingetoa ITC iende kwenye klabu inayomuhitaji.”
“Tunataka kumuona anakwenda kucheza nje ili awe professional kama wachezaji wengine wanaotoka Afrika kwenda kucheza Ulaya.”

No comments:

Post a Comment