tuwasiliane

Wednesday, November 23, 2016

Man United kumuongezea mkataba Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic ataongezewa mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Man United kulingana na meneja Jose Mourinho
Manchester United imesema kuwa itamuongezea kandarasi ya mwaka mmoja mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic kulingana na meneja Jose Mourinho.
Mchezaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35 alihamia Old Trafford katika uhamisho wa bure katika msimu huu akiwa na uwezo wa kuongeza kandarasi hiyo kwa msimu wa pili.Amefunga mabao 17 katika mashindano yote msimu huu.
Mourinho alisema: Tutaanda mpango wa kuongeza kandarasi yake kwa mwaka mwemgine .Baadaye anaweza kufanya atakacho.
Ibrahimoviv alisema: Najihisi vyema, nikiwa nitaendelea itakuwa mwaka mwengine.
Ibrahimovic aliyefunga mabao 62 katika mechi 116 akiichezea Sweden kabla ya kustaafu katika soka ya kimataifa mnamo mwezi Juni ,alikihama klabu cha PSG mwishoni ma msimu uliopita

No comments:

Post a Comment