tuwasiliane

Wednesday, November 23, 2016

Hussein Sharrif 'Casillas' mbioni kutimkia Ligi Kuu ya Congo DR

Hussein Sharrif - Kipa Kagera Sugar
Kipa  namba moja wa Kagera Sugar Hussein Shariffu maarufu kama 'Casillas' yupo mbioni kujiunga na klabu ya DC Motema Pembe ya DR Congo baada ya kocha wa timu hiyo kuvutiwa na kiwango chake.
Casillas  ambaye amesha wahi kucheza klabu za Simba na Mtibwa Sugar  kwa vipindi tofauti tofauti ameiambia tovuti ya Goal , viongozi wa timu hiyo ya DR Congo  wamemfuata na kumtaka akajiunge na timu yao kuanzia msimu ujao.
"Nimezungumza nao na kifupi nipo tayari isipokuwa nimewaambia wakazungumze na uongozi wa Kagera Sugar timu ambayo ina nimiliki hivi sasa," amesema Casillas.
Casillas hayupo na kikosi cha Kagera Sugar kwa muda mrefu baada ya kusimamishwa na uongozi wa timu yake, yeye na mchezaji mwenzake Peter Mganyizi wakituhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa viongozi wa klabu ya  Yanga na kusababisha kipigo cha mabao 6-2 katika mchezo wa Ligi ya Vodacom uliopigwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Kagera.
Endapo dili hili likikamilika atakuwa Mtanzania wa 3 kucheza Ligi Kuu ya DR Congo baada ya  Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu kuwahi kucheza Tp Mazembe  na Mussa Hassan Mgosi naye kuwahi kukipiga DC Motema Pembe  kuwahi kucheza huko kwa miaka ya hivi karibuni
DC Motema Pembe ambayo maskani yake ni Kinshasa nchini DR Congo inashika nafasi ya tatu Ligi Kuu ya Congo kanda ya Magharibi baada ya kujikusanyia alama 19 kwenye michezo 10  mpaka sasa huku wakiwa nyuma kwa pointi 2 dhidi ya  kinara wa ukanda wao klabu ya  Renaissance ambao wamejikusanyia pointi 21 kwa michezo 9 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi

No comments:

Post a Comment