tuwasiliane

Wednesday, November 30, 2016

Kiungo Matata sana wa Zesco atua Yanga

justine-zulu
Kiungo wa Zesco United Justine Zulu tayari ametua nchini akitokea Zambia kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Yanga.
Kwa namna yoyote, hayo ni mapendekezo ya kocha George Lwandamina ambaye tayari ameanza majukumu ya kuifundisha Yanga ambapo jana Jumatatu Novemba 28 alisimamia mazoezi ya klabu hiyo kwa mara ya kwanza akiwa kocha mkuu mpya aliyechukua nafasi ya Hans van Pluijm.
Kwa muda mrefu Yanga imekuwa na wachezaji wachache wa eneo la kiungo wa katikati (Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Juma Makapu na Mbuyu Twite) ukilinganisha na washindani wao wa ndani Simba na Azam FC ambao wanawachezaji wengi katika idara hiyo.
Justine Zulu anamiaka 27 amezaliwa 11 August 1989 Lusaka, Zulu amewahi kuvitumikaia vilabu vya National AssemblyHapoel Be’er ShevaHapoel Bnei LodHapoel Rishon LeZionEnosis Neon ParalimniLamontville Golden ArrowsKabwe Warriors na ZESCO United.
Mwaka 2012 alisaini miaka mitatu kuitumikia klabu ya Lamontville Golden Arrows ya Afrika Kusini. October 2013 alirejea kwenye ligi ya Zambia na kujiunga na  Kabwe Warriors, ukiwa ni mkataba wa muda mfupi. Baadae alijiunga na Zesco United kuelekea msimu wa 2014 ambapo ameendelea kuhudumu hadi sasa.
Mwaka 2011 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Zambia. Zulu alikuwa sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2012 lakini hakufanikiwa kutajwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 waliotwaa taji hilo mwaka 2012.
Wasifu wa Justine Zulu
Date of birth11 August 1989 (age 27)
Place of birthLusaka, Zambia
Height1.82 m (5 ft 11 12 in)
Playing positionMidfielder
Club information
Current teamZESCO United
Senior career*
YearsTeamApps(Gls)
2005–2007National Assembly
2007–2009Hapoel Be’er Sheva23(1)
2009–2010Hapoel Bnei Lod31(1)
2010–2012Hapoel Rishon LeZion50(3)
2012Enosis Neon Paralimni11(0)
2012–2013Lamontville Golden Arrows4(0)
2013Kabwe Warriors
2014–ZESCO United

No comments:

Post a Comment