Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka Jumatano kuelekea Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim
Kocha Hans van der Pluijm amekiambia chanzo chetu kuwa , maandalizi yoa yanakwenda vizuri na atautumia mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu Jumapili, kama kipimo kuelekea mchezo huo ambao amesema wanalazimika kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Pluijm amesema amewafanyia tathimini ya kutosha wapinzani wao na kubaini maandalizi waliyofanya ni sawa na hawahitaji kuongeza zaidi ya hapo kwani wanaweza kujichosha na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Yanga wanashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vodacom Tanzania msimu uliopita na sasa inaanza kibarua hicho dhidi ya Maurtius.
No comments:
Post a Comment