tuwasiliane

Monday, February 8, 2016

SABABU YA NDEMLA KUSUGUA BENCHI

Said Ndemla
Jackson Mayanja tangu atue Simba amegundua mapungu mengi na wachezaji wengine wenye uwezo kuwapa nafasi, Ndemla ni moja waliokosa nafasi, sababu nini?
Kocha wa Simba  Jackson Mayanja amesema sababu ya kumwanzisha benchi kiungo wa timu hiyo na Taifa Stars Said Ndemla, ni kutokana na mapungufu kidogo aliyokuwa nayo na sasa anamuandaa kwa ajili ya kumuimarisha ili acheze kwenye kiwango anacho kihitaji yeye.
Mayanja amekiambia chanzo kimoja kuwa, Ndemla ni mchezaji mzuri lakini kwenye mfumo wake amegundua anamapungufu hivyo ameona ambadilishe kwa kumuongezea vitu anavyo vihitaji ili aweze kumtumia kwasiku zijazo,”amesema Mayanja.
Kocha huyo amesema kama kocha anajua uwezo wa kila mchezaji wake na ndiyo mwenye jukumu la kupanga timu hivyo haoni sababu ya mashabiki wa Ndemla kuwa na hofu kwasababu binfasi yeye anamkubali mchezaji huyo ndiyo maana ameamua kuweka benchi akimtumia dadika za mwishoni ili kumbadilisha.
Ndemla analijua hilo na yeye amesema hana hofu na maamuzi ya kocha wake ispokuwa anaamini muda ukifika atacheza kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa enzi za utawala wa kocha Muingereza Dylan Kerr.

No comments:

Post a Comment