tuwasiliane

Monday, February 8, 2016

Manchester United yazungumza na Mourinho

Timu ya Manchester United imekataa kusema lolote juu ya madai kuwa ilifanya mashauriano na wawakilishi wa kocha mzoefu Jose Mourinho, aliyeachishwa kazi kutoka Chelsea Disemba, mwaka jana.
Habari za kuaminika hata hivyo zinasema kuwa mashauriano yamefanywa na Mourinho - ambaye ametajwa kama mmoja wapo wa makocha wanaowania kazi katika timu ya Manchester United ambayo imetapatapa kwa muda na ambayo kocha wake wa sasa, Lous Van Gaal, anatarajiwa kuondoka baadaye mwakani.
Hatua hiyo itampa fursa Mourinho ambaye anadaiwa kufurahia mapngo huo wakuifunza Manchester United.
Maafisa wa juu wa Man United wanatarajiwa kutoa jibu lao baada ya majirani zao Manchester City kuchukua huduma za Pep Guradiola ,mapema wiki hii.
Kuwasili kwa Mourinho kunamaanisha kwamba upinzani mkali utaanza kati ya City na United kufuatia ule uliokuwepo kati ya Real Madrid na Barcelona wakati makocha hao walipokuwa katika timu hizo mbili.
Katika kipindi cha wiki mbili kazi ya Van Gaal imekuwa ikiyumba yumba.
Hatahivyo,kushindwa kwa timu hiyo dhidi ya Stoke na Southampton kumesababisha kuimarika kwa timu hiyo.
United ambao wako pointi tano nyuma katika nafasi ya kufuzu kwa michuano ya kilabu bingwa Ulaya itacheza dhidi ya Chelsea siku ya jumapili.

No comments:

Post a Comment