Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Michael Olunga ambaye alitoa ombi kwa kilabu ya Arsenal kumsajili mwaka uliopita amejiunga na kilabu ya Djurgardens ya Sweden kutoka kilabu ya Gor Mahia.
Mchezaji huo mwenye umri wa miaka 21 alichapisha kanda ya video mwezi Agosti akimtaka kocha wa Arsenal Arsene Wenger kumsajili.
Badala yake amejiunga na kilabu Djurgardens kwa kandarasi ya miaka minne baada ya kujaribiwa kwa mwezi mmoja.''Yuko kabambe na ana lengo,anafanya sana mazoezi na kila mara anataka kujifunza na kuchukua hatua nyengine,''mkurugenzi wa michezo katika kilabu hiyo Bosse Andersson amesema.
''Anaendelea vizuri na ana uwezo wa kuwa mshambuliaji ambaye anaweza kuichezea timu yoyote katika ligi za Ulaya kutokana na mazingira yetu mazuri''.Olunga aliyepewa jina la utani kama Engineer kutokana na elimu yake ya chuo kikuu na talanta yake ya soka amekiri kwamba anaendelea kujifunza.
''Mara ya kwanza lazima nianze polepole,lakini ninapoendelea kujifunza ninaendelea kupata mabao mengi,aliuambia mtandao wa kilabu hiyo.Kufikia sasa nimecheza mechi za kirafiki lakini najihisi vyema.
No comments:
Post a Comment