tuwasiliane

Friday, February 19, 2016

Hatutobadili mfumo wa 3-5-2 '- Stewart Hall

'Hatutobadili mfumo wa 3-5-2 '- Stewart Hall
Azam wamepoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya Coastal Union
Kocha wa klabu ya Azam FC Stewart Hall amesema ni vigumu kwa sasa timu hiyo kubadili mfumo wa 3-5-2 kipindi hiki kutokana na kuhofia kuwachanganya wachezaji ingawa wapinzani wao wengi wakiwa wamewajulia.
Hall amekiambia chanzo chetu, mbinu hiyo ndiyo imewasaidia kucheza mechi 13 za ligi bila kufungwa na ndiyo waliyoitumia kubeba ubingwa wa Kombe la Kagame Julai 2015 hivyo siyo rahisi kuiacha kirahisi .
“Najua kweli timu nyingi zimetusoma na kujua mipango yetu lakini hatuwezi kubadili wakati ligi ipo kwenye ushindani na tunataka ubingwa chamsingi tutakuwa tunabadili vitu vidogo vidogo kuhakikisha tunapata ushindi na baada ya msimu kuisha ndiyo tuta jifunza mbinu mpya,”amesema Hall.
Kutokana na timu nyingi kuwabaini mfumo wanaotumia wiki iliyopita Azam walijikuta wakipoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya Coastal Union.

No comments:

Post a Comment