tuwasiliane

Wednesday, January 6, 2016

ZIDANE AKABIDHIWA KAZI YA KUMPA STRESS

Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtimua kocha wake Rafael Benitez ambaye amehudumu miezi 7 pekee.
Sasa nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha Real Madrid .
Hii inatokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka sare 2-2 na Valencia, katika Mechi ya La Liga, sare ambayo imewaacha vigogo hao nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.
Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa hapendwi na Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico mwezi Novemba na mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.

Rekodi ya Rafa Benitez

Real Madrid wamemfuta kazi

3
Nafasi ya Real kwa sasa La Liga
  • 4 Alama walizo nyuma ya viongozi Atletico Madrid
  • 7 miezi aliyohudumu mkataba wake wa miaka 3
  • 1 Mchezaji asiyefaa(Denis Cheryshev) aliyechezeshwa Copa del Rey - na kufanya Real Madrid kuondolewa michuano hiyo
Getty
Aidha, klabu hiyo ilitupwa nje ya Copa del Rey baada ya kumchezesha mchezaji asiyestahili katika mechi dhidi ya Cadiz.
Hali hiyo imefanya kuwepo minong’ono ya kila mara kuwa wachezaji wa Real hawana raha na Benitez na wana mgomo baridi dhidi yake.
Wiki iliyopita Benitez aliwatuhumu wanahabari kwa kuendesha kampeni ya kumpinga yeye, klabu na rais wao Florentino Peréz.

No comments:

Post a Comment