tuwasiliane

Saturday, January 16, 2016

SIMBA VS MTIBWA MWENDO WA KULIPIZA KISASI TU LEO TAIFA

Preview Simba-Mtibwa Sugar, Msimbazi kulipa kisasi
Kocha mpya wa Simba Jackosn Mayanja leo atakuwa na mtihani wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo siku tano zilizopita wakati atakapo pambana na washindi wa pili wa Kombe la Mapinduzi Mtibwa Sugar hilo likiwa pambano la Ligi ya Vodacom litakalopigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali hasa kwa wenyeji Simba ambao wiki moja iliyopita walifungwa na kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi na Mtibwa Sugar hivyo kesho itataka kulipa kisasi huku ikiongozwa na kocha mpya Mayanja aliyeletwa kama kocha msaidizi kumsaidia Dylan Kerr ambaye hayupo tena kwenye timu hiyo baada ya kufukuzwa kufuatia kipigo cha Mtibwa.
Timu hizo zinakutana zote zikiwa katika nafasi ya tatu zikifungana kwa pointi 27, kila moja lakini Simba wakiwa juu nafasi ya tatu kutokana na idadi kubwa ya mabao ya kufunga tofauti na Mtibwa Sugar.
Mayanja ameanza kwa kasi kibarua chake lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa na subra wakati akiijenga timu hiyo kabla ya kuanza kufurahia matunda mazuri na hilo amesema halita chukua muda mrefu kutokana na vipaji walivyonavyo wachezaji aliowakuta.
Mayanja amekaririwa akisema kuwa Mtibwa ni timu ya kawaida na wanatarajia kuibuka na ushindi, huku akiomba wapenzi wa timu hiyo kuwaunga mkono kwa kufika kwa wingi uwanjani kwenda kuiona Simba mpya itakayokuwa chini yake.
Mganda huyo aliyewahi kuzifundisha timu za Kagera Sugar na Coastal Union, amesema anawajua vizuri wapinzani wao lakini kufanya vizuri kwao kwenye michuano ya Mapinduzi hakumpi hofu na kumfanya akose usingizi akiwaza mchezo huo.
“Nimezungumza na wachezaji wangu na kuwaeleza umuhimu wa ushindi wote wamenihakikishia kupata pointi tatu na ndiyo kitu cha msingi kwangu na kwa mashabiki wetu ambao wanaonekana kukata tamaa kwasababu Simba ni timu kubwa na haikuwa ikiwapa furaha msahabi wake,”amesema.
Kwa upande wake kocha Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar, amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo huo wa leo na kwamba hawahofii Simba kwasababu ni moja ya timu 16, zilizopo kwenye ligi ya Vodacom ambazo nilazima acheze nazo.
Maxime anasema mchezo utakuwa mgumu kwa timu zote mbili kwasababu wenyeji wao Simba watacheza kwa nguvu kutaka kulipa kisasi cha kuwafunga bao 1-0, Zanzibar na wao hawapo tayari kupoteza mchezo huo kwa sababu wanataka kuendeleza rekodi yao mzuri msimu huu ya kutotoka nje ya tatu bora.
“Watakuja kwa kasi hasa ukiangalia wapo chini ya kocha mpya lakini tumejiandaa mazoezi ya siku mbili tuliyofanya naamini yatatusaidia kurudi nyumabani na pointi tatu lakini pia tukiwa na matokeo mazuri ya kombe la Mapinduzi,”amesema Maxime.

No comments:

Post a Comment