tuwasiliane

Saturday, January 16, 2016

MOISE KATUMBI AZIDI KUMLETEA FIGISU FIGISU SAMATTA KWENDA GENK

katu
Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe Moise Katumbi amegeuka wakala baada ya kuweka majukumu yake pembeni na kuanza kumtafutia timu nyota wa timu hiyo Mbwana Samatta ili akacheze kwenye timu ambayo anataka yeye (Katumbi) na siyo timu ambayo inamuhitaji Samatta au timu ambayo anataka kucheza Samatta.
Sakata hilo limekuja baada ya klabu ya Genk ya Ubeligiji kukubaliana kila kitu na star huyo wa Bongo lakini boss huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekuwa akitia ngumu kumwachia Samatta kwa sababu zake binafsi.
Picha lilianza hivi, klabu ya Genk ilisha kubaliana kila kitu na Samatta na kilichokuwa kikisubiriwa ni Katumbi kutoa baraka zake ili klabu hiyo imalizane na Mazembe na kuinasa siani ya mchezaji huyo aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.
Katumbi alianza kutaja bei kubwa za kumuuza Samatta kwa makusudi ili klabu hiyo ishindwe kumnunua nyota huyo ambaye amebakiza miezi mitatu ili mkataba wake na Mazembe umalizike. Dau ambalo limekuwa likitajwa na Katumbi limekuwa haliendani na mkataba ambao umebaki kati ya Samatta na Mazembe lakini boss huyo amekua akikomaa ili dili hilo lifeli na Samatta aendelee kubaki Mazembe.Katika kuhakikisha anatimiza dhamira yake ya kumfelisha Samatta kujiunga na Genk, Katumbi alisafiri hadi nchini Ufaransa na kukutana na klabu ya Nantes na kucheza nao dili la kuhakikisha safari ya Samatta inafeli na anaendelea kusalia Mazembe.
Alichokifanya Katumbi ni kucheza mchezo na Nantes, akawaambia wapeleke offer TP Mazembe kwamba wanamuhitaji Samatta akacheze kwenye klabu yao wakati huo klabu hiyo haina mpango kabisa Samatta. Akaenda mbali zaidi na kuwaambia yeye ndiye atalipia gharama zote za usajili wa Samatta kutoka Mazembe kwenda Nantes.
Kwa kuwa klabu hiyo haimuhitaji Samatta, isinge mtumia hata kidogo kwasababu hayupo kwenye mipango yao kwahiyo atajikuta nje ya timu hiyo hali ambayo itapelekea akumbuke maisha ya Mazembe kitu ambacho Katumbi anakiota.
Akishindwa maisha ya kusugua benchi atapewa poption ya kurudi Mazembe kitu ambacho ni lengo la Katumbi na atakua amefaulu mchezo wake kwa 100%.
Ili kuhakikisha hilo linatimia, Katumbi alisafiri kutoka Congo DR mpaka Bongo na kuja kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Shirikisho nla soka la Tanzania (TFF) (majina tunayo) ili wajaribu kumshawishi Samatta akubali kwenda Ufaransa na si Ubeligiji. Kwasababu Samatta anajua nini kinaendelea, na yeye akawatolea mbavuni.
Samatta ameustukia mchezo huo mchafu unaochezwa na Katumbi ambaye ameanza kushirikiana na baadhi ya viongozi wa TFF kuhakikisha anafeli kwenda Genk na hatimaye ajiunge na Nantes ili mwisho wa siku ashindwe maisha ya kwenye klabu hiyo na kuona ni bora arudi Mazembe kuliko kuendelea kusulubika Ufaransa.
Klabu ya Genk ilionesha nia ya kumuhitaji Samatta mapema na ilifuata taratibu zote, zinazohitajika. Kawasababu mkataba wa mchezaji huyo na timu yake upo chini ya miezi sita, taratibu na kanuni za FIFA zinaruhusu mchezaji husika kuzungumza na timu yeyote inayomhitaji.
Viongozi wa Genk walifunga safari kutoka Ubeligiji hadi Dar wakakutana na uongozi wa Samatta na kufanya mazungumzo lakini kama vile haitoshi, walisafiri hadi Japan ili kuonana na Samatta wakati huo klabu ya Mazembe ilikuwa nchini humo kwa ajili ya michuano ya FIFA Club World Cup. Viongozi hao walikutana na Samatta kisha kufanya nae mazungumzo na kukubaliana mambo kadha wa kadha kwa pande zote mbili.
Baada ya kila kitu kwenda sawa ndipo wakakutana na Katumbi kumpelekea offer ambayo mwanzoni alikubaliana nao kila kitu. Lakini badaye boss huyo akawa haeleweki na kuanza kutaja bei za ajabu za kumuuza Samatta kitu ambacho kiliwastua Genk. Kumbe lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha klabu hiyo inashindwa kumnasa mshambuliaji wake.
SOURCE SHAFFIH DAUDA

No comments:

Post a Comment