tuwasiliane

Friday, January 1, 2016

Nadir Haroub: "Niyonzima ameacha pengo Yanga"

Nadir Haroub 'Cannavaro'
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kumkosa kiungo Haruna Niyonzima kwenye kikosi chao ni pengo kubwa ambalo litachukua muda mrefu ili kuweza kuliziba.
Cannavaro aliyebakiza siku chachhe kurejea dimbani akitoka kuuguza majeruhi ya mguu yaliyosababisha afungwe P O P, na kukosa mechi tano za karibuni amekiambia chanzo chetu kuwa, mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda, alikuwa na mchango mkubwa kwao hivyo kuondolewa kwake kunaweza kuiyumbisha timu katika harakati za kutetea ubingwa wao wa Ligi ya Vodacom Tanzania.
“Ukweli inaumiza kwa sababu Niyonzima kwanza alikuwa msaidizi wangu lakini alikuwa na mchango mkubwa kwetu ndani na hata nje ya uwanja lakini siwezi kusema sana kwa sababu haya yameshatokea na uongozi umeamua kutoa adhabu yake kulingana na vifungu vilivyo kwenye mkataba sina budi kukubaliana na hali iliyopo,” amesema Cannavaro.
Beki huyo anayecheza kwa kujituma na tegemezi kwa Yanga amesema katika misimu mitano ambayo amecheza na nyota huyo ameweza kujifunza mambo mengi kutoka kwake ikiwemo utulivu hata katika mechi ngumu za kiataifa ambazo zilisaidia wao kupata ushindi.
Mapema wiki hii uongozi wa Yanga uliamua kuvunja mkataba wa miaka miwili na niyonzima, kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kuchelewa kujiunga na timu wakati ikielekea Jijini Tanga Desemba 12 kucheza mechi za ligi ya Vodacom dhidi ya Mgambo JKT na African Sports na mechi yake ya mwishosho kuvaa jezi za Yanga ilikuwa ni katika mchezo wa Kagera Sugar uliopigwa uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora.

No comments:

Post a Comment