tuwasiliane

Wednesday, January 6, 2016

Liverpool yaichapa Stoke-capital one.

Klabu ya soka ya Liverpool hapo jana ilifanikiwa kuifunga stoke city bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Nusu fainali ya michuano ya Capital One katika mchezo uliopigwa dimba la Brittania.
Bao pekee la ushindi la Liverpool limefungwa na mchezaji Jordon Ibe katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza ushindi ambao umempa furaha kocha wake Jurgen Klopp na kumpa matumaini ya kutinga fainali ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo sasa Liverpool huenda ikakutana kati ya Everton au Manchester City mchezo ambo utafanyika katika uwanja wa Wembley.
Mchezo mwigine wa nusu fainali ya kwanza unatarajia kupigwa usiku wa leo ambapo Everton watakuwa nyumbani Goodson Park dhidi ya Mnchester city.

No comments:

Post a Comment