tuwasiliane

Wednesday, December 9, 2015

TP MAZEMBE KUANZA MICHUANO YA KLAB BINGWA YA DUNIA JUMAPILI IJAYO

Mazembe
Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe wamewasili mjini Osaka, Japan jana kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.Timu hiyo iliwasili mjini Osaka japan ikiwa na nyota wake wote,kama Mbwana samatta na Thomas Ulimwengu kutoka Tanzania na Kalaba,na wakali wengine
Michuano hiyo itakayoanza kesho.
Vijana hao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walishinda kombe la klabu bingwa Afrika mwezi uliopita.
Wataanza kampeni yao Osaka Jumapili dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Sanfrecce Hiroshima na Auckland City FC ambayo itachezwa Alhamisi.
Mazembe walishangaza ulimwengu miaka mitano iliyopita walipofika fainali ya dimba hilo la dunia lakini wakashindwa na Inter Milan.

No comments:

Post a Comment