tuwasiliane

Thursday, December 10, 2015

Louis van Gaal hana kisingizio

Bosi wa Manchester United Louis van Gaal amesema hana kisingizio chochote cha kwanini wametolewa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na sasa kucheza UEFA EUROPA LIGI.
Hii ni mara ya 4 kwa Man United kushindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UCL baada ya Jana kuchapwa 3-2 na Wolfsburg na kushushwa Nafasi ya 3 ya Kundi B na hivyo kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Licha ya kushindwa kuvuka toka Kundi B ambalo Wachambuzi walihisi kuwa ni jepesi kwani Timu nyingine zilikuwa PSV Eindhoven na CSKA Moscow, Louis van Gaal amesisitiza Man United iko kwenye njia sahihi chini yake.
United iko katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu, wakiwa walimaliza katika nafasi kama hiyo katika msimu wa kwanza wa Van Gaal.

No comments:

Post a Comment