tuwasiliane

Wednesday, December 9, 2015

HANS POPPE AVUNJA UKIMYA,ASEMA KESSY YUKO HURU KUJIUNGA NA KLAB ANAYOIPENDA

Hassan Ramadhani wa Simba amekuwa akisita kusaini mkataba mpya kuendelea kubaki Msimbazi. Uongozi wa Simba umefunguka sasa.
Hassan Kessy | Simba
Uongozi wa klabu ya Simba umesema hautakuwa na haraka kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba wa beki wake wa kulia Hassan Ramadhan ‘Kessy’ aliyebakiza miezi sita kumaliza mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, amekiambia chanzo chetu, bado kuna muda mrefu wa kufanya mazungumzo na mchezahu huyo hivyo haoni haraka ya kutaka kumchanganya wakati timu yao kwasasa ipo katika maandalizi muhimu kujiandaa na mechi za ligi zinazotarajia kuendelea Jumamosi ya Desemba 12.
“Najua kama ana uhuru wa kufanya mazungumzo na klabu nyingine lakini sisi hatuliofii hilo, kwasababu bado nimchezaji wa Simba kwa sasa na atakuwa huru baada ya kuisha kwa miezi sita na katika kipindi chote hicho naamini tutakaa naye na kufanya mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya,”amesema Hans Poppe.
Poppe amesema wanachokifanya kwasasa ni kutoa nafasi kwa mchezaji huyo kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua timu anayoipenda ili aweze kuichezea kipindi kijacho.
Kessy alisajiliwa Simba msimu uliopita kutoka Mtibwa Sugar, anatarajiwa kumaliza Mkataba wake Juni mwakani lakini kumekuwa na tetesi kwamba mchezaji huyo anampango wa kujiunga na timu nyingine.

No comments:

Post a Comment