tuwasiliane

Tuesday, February 10, 2015

Yanga, Azam tayari kwa El-Merreikh

                    
Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya vilabu ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF), Yanga na Azam wamesema maandalizi yamekamilika kwa ajili ya mechi zao za wikiendi hii dhidi ya El-Merreikh ya Sudan na BDF XI ya Botswana jijini Dar es Salaam.
Wakati mtendaji mkuu wa klabu ya Azam, Saad Kawemba akisema maandalizi katika uwanja wao wa nyumbani, Chamazi yamekamilika kwa ajili ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Wasudan katika kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga wamesema wameanza kambi maalumu na kuomba mashabiki kuhudhuria kwa wingi.
Yanga itacheza na BDF ya Botswana, siku hiyo hiyo ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mkuu wa Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro amesema wanategemea kuibuka na ushindi.
“ Tunawaomba mashabiki kuja kwa wingi uwanjani ili kuipa nguvu timu”, amesema Muro, huku akitaja kiingilio cha chini kabisa kuwa Sh5,000 (wastani wa dola 3) ili kuwawezesha mashabiki wengi kuingia uwanjani.
Mechi za marudiano kati ya timu hizo zitafanyika bada ya wiki mbili mjini Khartoum-Sudan ( Azam vs El-Merreikh) na Gaborone-Botswana (Yanga vs BDF).

No comments:

Post a Comment