tuwasiliane

Saturday, October 25, 2014

CHID BENZ AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AIRPORT




Kamanda Nzowa amesema kuwa Chid amekutwa na madawa hayo baada ya upekuzi wa kawaida uliokuwa ukiendelea uwanjani hapo, ambapo jeshi la polisi linamshikilia kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Mara baada ya kupata taarifa hizo,mtandao huu uliwasiliana na Kamanda Nzoa ambaye alifunguka kama ifuatavyo:
“Ni kweli tumemkamanda Rashid Makwiro maarufu kwa jina la Chid Benz akiwa na kete kumi na nne za madawa ya kulevya aina ya heroine pamoja na misokoto miwili ya bangi.
“Msanii huyo alikuwa njiani kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki, na sasa amewekwa katika sehemu maalum ambayo hatuwezi kusema ni wapi, kwa sababu za kiusalama, uchunguzi wa tukio unaendelea.”
Taarifa zilizokuwepo awali zilisema kuwa Chid alikuwa njiani kwenda Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye shoo ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.
Chid ni kiongozi wa kundi la muziki la la Famila lenye makao makuu Ilala jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment