tuwasiliane

Wednesday, September 24, 2014

Obama aapa kuangamiza Islamic State


Rais wa Marekani Barack Obama amesema Marekani itashambulia kundi linalojiitaa Islamic state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima kabisa makao ya kujificha .

Bw Obama amesema kushiriki kwa mataifa kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo kunaonyesha wazi hivyo si vita vya Marekani pekee bali wao ni sehemu ya muungano wa mataifa yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia ISIL.

Pia amekiri kuwa mashambulio hayo yamelenga pia wale aliowataja kuwa wanamgambo sugu wa al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao anasema wanalenga kuishambulia Marekani.

Nazo taarifa za jeshi la Marekani zasema malengo ya mashambulio yaliyofanywa yametimia.


Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander Lukashevichy amesema mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti yazingatie sheria za kimataifa.
Kadhalika Obama, amesema kuwa kuhusika kwa nchi za kiarabu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria ni dalili toshja kuwa vita hivi sio vya Marekani pekee.

Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu,Jordan na Bahrain zote zilituma ndege za kijeshiu katika opereshei hiyo.

No comments:

Post a Comment