Shirika la Ndege la Falme za Ghuba, Emirates, lenye
makao yake Dubai, limesimamisha kwa muda safari za ndege za kwenda
Guinea kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola ambao umeuwa zaidi ya watu 700
Afrika magharibi mwaka huu.
Katika tovuti yake Emirates imesema haiwezi kutia hatarini afya ya abiria na wafanyakazi wake.Homa ya Ebola ilianza Guinea na kutapakaa nchi jirani za Sierra Leone na Liberia.
Mashirika mawili ya ndege ya Afrika, (Arik Air, ya Nigeria, na ASKY ya Togo,) yameshatangaza kuwa yamevunja safari za kwenda nchi zilizoathirika.
Shirika la ndege la Emirates halina safari za kwenda Sierra Leone au Liberia.
No comments:
Post a Comment