tuwasiliane

Tuesday, July 1, 2014

YANGA YAANZA KAZI UFUKWENIKikosi cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika Ufukwe wa Coco Beach chini ya kocha mkuu mpya mbrazil Marcio Maximo tayari kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015 na mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans imeanza rasmi maandalizi ya msimu mpya chini ya kocha mpya Maximo ambaye alijijengea heshima kubwa miaka minne iliyopita wakati alipokuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) kutokana na falsafa yake ya soka la vijana na kusimamia nidhamu.

Jumla ya wachezaji 14 kutoka timu ya wakubwa wamehudhuria mazoezi ambapo leo kikubwa walikua wakifanya mazoezi ya kusaka pumzi, kujenga mwili huku baadhi ya washabiki wakijitokeza kushuhudia mazoezi ya mbrazil huyo.
Wachezaji waliofanya mazoezi leo ni:
1.Ally Mustafa "Barthez" 2.Juma Abdul, 3.Swaleh Abdallah, 4.Rajab Zahir, 5. Mbuyu Twite, 6.Salum Telela, 7.Omega Seme, 8.Hassan Dilunga, 9.Said Bahanuzi, 10. Andrey Coutinho, 11.Hussein Javu, 12.Juma Kaseja, 13.Nizar Khalfani, 14.Jerson Tegete
Katika mazoezi ya leo kocha Maximo ameendelea kuwakosa wachezaji 11 ambao wapo katika timu za Taifa mbali mbali wakijiandaa na michezo itakayowakabili mwishoni mwa mwezi huu, wakipigania kucheza fainali za Mataifa Afrika.
Wachezaji walio kwenye timu ya Taifa Tanzania ni 1.Deo Munish "Dida", 2.Oscar Joshua, 3.Kelvin Yondani, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Saimon Msuva, 6.Mrisho Ngasa, 7.Pato Ngonyani, 8. Said Juma huku Uganda ikiwa na Emmanuel Okwi, na Hamis Kizza na Rwanda Haruna Niyonzima.
Mara baada ya mazoezi ya asubuimu iliendelea na mazoezi kwenye uwanja wa bandari- tandika
source.www.youngafricans.co.tz

No comments:

Post a Comment