ZIKIWA
zimesalia dakika mbili mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti baada
ya Argentina na Uswisi kuwa hazijafungana katika mchezo wa 16 Bora Kombe
la Dunia jioni hii Brazil, Angel di Maria alifanya mambo.
Nyota
huyo wa Real Madrid aliitendea haki pasi nzuri ya Lionel Messi wa
Barcelona dakika ya 118 kuipeleka Argentina Robo Fainali ya Kombe la
Dunia.
Tofauti
na ilivyotarajiwa akina Messi wangefuzu kiulaini, Uswisi waliibana
Argentina na ilibaki kidogo mshindi aamuliwe kwa matuta.
Kikosi
cha Argentina kilikuwa; Romero, Federico Fernandez, Zabaleta, Garay,
Rojo/Basanta dk105+1, Gago/Biglia dk106, Mascherano, Di Maria, Higuain,
Messi na Lavezzi/Palacio dk74.
Uswisi;
Benaglio, Lichtsteiner, Schar, Djourou, Rodriguez, Inler, Behrami,
Xhaka (Fernandes 66), Shaqiri, Mehmedi/Dzemaili dk113 na Drmic/Seferovic
dk82.
No comments:
Post a Comment