Shirikisho la Kandanda la Dunia, FIFA, limeionya
Nigeria kwamba itatolewa katika kandanda ya kimataifa iwapo serikali
haitalirejesha tena shirika la kandanda la Nigeria, Nigerian Football
Federation, ifikapo Jumaane juma lijalo.
FIFA imesema imetiwa wasi-wasi na hatua ya serikali ya Nigeria dhidi ya chama cha kandanda cha nchi hiyo.
Kanuni za FIFA zinaeleza wazi kuwa wanachama wake lazima waruhusiwe kufanya kazi yao bila ya kuingiliwa kati na serikali.
Wakuu wa Nigeria wamekifuta chama cha kandanda cha taifa na piya kumkamata rais wa chama; na waziri wa michezo amemteua mkurugenzi wake kuongoza chama hicho.
Haijulikani sababu ya serikali ya Nigeria kufanya hivyo.
Lakini iwapo serikali haitabadili uamuzi wake basi Nigeria haitaweza kushiriki katika mechi za kimataifa, mazoezi na kadhalika.
No comments:
Post a Comment