tuwasiliane

Saturday, June 21, 2014

UINGEREZA YATUPWA NJE KWENYE KOMBE LA DUNIA MAPEMA ZAIDIUingereza wameondolewa kutoka kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil baada ya raundi ya kwanza, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.
Uingereza ilibanduliwa baada ya Italia kupoteza mechi yao dhidi ya Costa Rica 1-0 huko Recife katika kundi D.
Uingereza ilikuwa imeshindwa na Uruguay na Italia katika mechi zilizotangulia.
Uingereza ilihitaji Italia kushinda mechi yao ili wapate matumaini ya kuendelea lakini Costa Rica walipoishinda Italia, matumaini yao yakapotea pia.

No comments:

Post a Comment