tuwasiliane

Sunday, June 29, 2014

UHOLANZI YATINGA ROBO FAINALI,YAIPIGA MEXICO 2-1

 Level: Wesley Sneijder scored in the 88th minute to drag Holland bag into the gameUHOLANZI imeenda Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Mexico mabao 2-1 ikitoka nyuma kwa 1-0 jioni hii nchini Brazil.

Shkurani kwake, Klaas-Jan Huntelaar aliyefunga kwa penalti bao la ushindi dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, baada ya Arjen Robben kuangushwa kwenye boksi  na Marquez.
 Awali ya hapo, Wesley Sneidjer aliifungia bao la kusawazisha Uholanzi dakika ya 88 kufuatia 

Giovani dos Santos kutangulia kuifungia Mexico dakika ya 48. Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Vlaar, De Vrij, Verhaegh/Depay dk56, Kuyt, Wijnaldum, De Jong/Martins Indi dk9, Blind, Sneijder, Robben na Van Persie/Huntelaar dk76.

Mexico: Ochoa, Aguilar, Rodriguez, Marquez, Moreno/Reyes dk46, Layun, Salcido, Herrera, Guardado, Giovani/Aquino dk61 na Peralta/Hernandez dk75.

No comments:

Post a Comment