tuwasiliane

Sunday, June 29, 2014

MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI SIMBA,AVEVA AMESHINDA URAIS,KABURU UMAKAM WA RAIS

 Matokeo ya awali ambayo Blog hii  imeyapata kutoka chumba cha kuhesabia kura ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, Evans Elieza Aveva ameshinda Urais kwa kupata kura 1452 kati ya 1845 zillizopigwa, mpinzani wake Andrew Tupa akipata kura 387 wakati kura sita zimeharibika. Hata hivyo, matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro baadaye.
wakati huo Geoffrey Nyange 'Kaburu' ameshinda Umakamu wa Rais Simba SC baada ya kupata kura 1043 akimshinda mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo ni taarifa za awali, matokeo kamili yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi baadaye.huo;

No comments:

Post a Comment