Bao la kichwa la John Brooks, katika dakika za
mwisho za mechi ziliisaidia Marekani kuilaza Ghana kwa mabao mawili kwa
moja, katika mchuano wao wa kwanza wa kundi G, huko Natal.
Clint Dempsey alikua ameipa Marekani bao la kwanza chini ya dakika moja mchuano ulipoanza; Baada ya sekunde 31 pekee.Marekani imelipiza kisasi kushindwa na Ghana katika mkondo wa mchujo kwenye kombe la dunia la mwaka 2010, Afrika Kusini.
Jozy Altidore angeongezea uongozi wa Marekani katika dakika ya kumi na tisa ila mkwaju wake ulizuiwa na kipa wa Ghana.
Altidore aliondolewa baadaye katika mechi hiyo baada ya kujeruhiwa.
Yawezekana kuwa hataweza kuichezea Marekani tena katika michuano iliyosalia ya kombe la dunia mwaka huu.
Kikosi hicho kitasalia na wachezaji 22 kwa michuano yao inayokuja kwani sheria za Fifa zinazuia wachezaji wengine kuongezwa katika kikosi baada ya kuanza kwa mashindano.
Ghana ingesawazisha kabla ya mapumziko wakati Christian Atsu alipompatia Jordan Ayew pasi nzuri.
Hata hivyo Ayew, anayeichezea timu ya Marseille huko Ufaransa, alitoa mwaju hafifu.
Katika kipindi cha pili, Ghana ilianza kutafuta bao la kusawazisha.
Asamoah Gyan alipewa nafasi nzuri ya kufanya hivyo lakini alipogeuka ili kuuondoa mpira, Geoff Cameron, wa Marekani alikua tayari keshafika na kulizuia jaribio hilo lake Gyan.
Marekani ilizidisha shinikizo lao la kutafuta bao la pili, hata hivyo Ghana ikatangulia kwa kusawazisha mnamo dakika ya 82, pale ambapo pasi yake Gyan, ilimfikia Andre Ayew naye bila kusita akautia mpira wavuni.
Wachezaji wake mkufunzi, Jurgen Klinsmann, waligeuka na kuanza kutafuta bao la ushindi kwa dhati.
Graham Zusi alimpa pasi mchezaji wa akiba Brooks, kutoka kwenye kona.
Brooks aliugonga kwa kichwa mpira nao ukaingia wavuni katika dakika ya 86 na kuipa Marekani uongozi tena. Marekani ilidhibiti lango lao kwa dakika tano za ziada na kupata ushindi dhidi ya Ghana.
Mpira wa kichwa kutoka kwa John Brooks, katika dakika za mwisho za mechi ziliisaidia Marekani kuilaza Ghana kwa mabao mawili kwa moja, katika mchuano wao wa kundi G, huko Natal.
Awali, Clint Dempsey alikua ameipa Marekani bao la kwanza chini ya dakika moja mchuano ulipoanza; Baada ya sekunde 31.
Hili ndilo lililokuwa bao la kasi kabisa katika historia ya taifa hilo katika kombe la dunia.
Marekani imekipiza kisasi kushindwa na Ghana katika mkondo wa mchujo kwenye kombe la dunia la mwaka 2010, afrika Kusini.
Jozy Altidore angeongezea uongozi wa Marekani katika dakika ya kumi na tisa ila mkwaju wake ulizuiwa na kipa wa Ghana.
Altidore aliondolewa katika mechi hiyo baada ya kupata jeraha.
Yawezekana kuwa hataweza kuichezea Marekani tena katika michuano yao iliyosalia ya kombe la dunia mwaka huu.
Kikosi hicho kitasalia na wachezaji 22 kwa michuano yao inayokuja kwani sheria za Fifa zinazuia wachezaji wengine kuongezwa katika kikosi wakati huu.
Ghana ingesawazisha kabla ya mapumziko wakati Christian Atsu alipompatia Jordan Ayew pasi nzuri
Hata hivyo Ayew, anayeichezea timu ya Marseille huko Ufaransa, alitoa mwaju hafifu.
Katika kipindi cha pili, Ghana ilianza kutafuta bao la kusawazisha.
Asamoah Gyan alipewa nafasi nzuri ya kufunga bao lakini alipogeuka ili kufyatua kombora , Geoff Cameron, wa Marekani alikua tayari keshafika na kuzima azimio lake .
Marekani ilizidisha shinikizo lao la kutafuta bao la pili, hata hivyo Ghana ikatangulia kwa kusawazisha katika dakika ya 82, pale ambapo pasi yake Gyan, ilimfikia Andre Ayew naye bila kusita akautia mpira wavuni.
Wachezaji wake mkufunzi, Jurgen Klinsmann, waligeuka na kuanza kutafuta bao la ushindi kwa dhati.
Graham Zusi alimpa pasi mchezaji wa akiba Brooks, kutoka kwenye kona.
Brooks aliugonga kwa kichwa mpira nao ukaingia wavuni katika dakika ya 86 na kuipa Marekani uongozi tena.
Marekani ilidhibiti lango lao kwa dakika tano za ziada na kulipiza kisasi kushindwa na black stars katika mashindano mawili ya kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment