tuwasiliane

Wednesday, June 25, 2014

KWA KITENDO HIKI,SUAREZ INABIDI APELEKWE KWA WASHAURI NASAHA

Fifa investigating Suarez bite

Mshambulizi wa Uruguay Luis Suarez amekumbwa na kashfa mpya baada ya kuonekana kumngata Giorgio Chiellini wa Italia.
Suarez alionekana akiminya bega la Chiellini muda mchache kabla ya Diego Godin kufunga bao la ushindi la Uruguay dhidi ya Italia.
Chiellini aliangushwa chini na uchungu wa meno ya Suarez na alionekana akimkimbilia refarii akimvulia shati ilikuonesha alama ya meno begani lakini refarii akapuzilia mbali .
Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.

 
Japo refarii Marco Rodriguez hakuona tukio hilo la kutamausha Chiellini amesikika akisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuwa refarii huyo alipuzilia mbali maombi yake ya kutaka hatua ichukuliwe dhidi ya mshambulizi huyo ambaye aliadhibiwa kwa tukio lengine kama hilo akiichezea Liverpool misimu miwili iliyopita nchini Uingereza.
Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumngata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013.
Awali Suarez aliadhibiwa na shirikisho la soka la Uholanzi lilimuadhibu Suarez kwa marufuku ya mechi saba baada ya kumngata mchezaji wa PSV Eindhoven Otman Bakka wakati huo akiwa nahodha wa Ajax Amsterdam.
Mwaka wa 2010 Suarez aliunawa mkwaju ambao ulikuwa unaingia wavuni na kuinyima Ghana nafasi ya kuingia kwenye nusu fainali ya kombe la dunia .
Kwa kitendo hiki cha kumng`ata tena mchezaji tena kwenye kombe la dunia,FIFA inabidi imchukulie hatua kali Suarez,kwani si kitendo cha kibinadamu kabisa.Pia Suarez apelekwe kwnye Clinic  za Masychologist ili aweze kupewa ushaur nasaha

No comments:

Post a Comment