tuwasiliane

Monday, June 16, 2014

BENZEMA APIGA MBILI UFARANSA IKIUA 3-0 KOMBE LA DUNIA

 

Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufaidi matumizi ya teknolojia ya kisasa kuzuia ubishi katika mechi ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.
Karim Benzema alikuwa anatekeleza mashambulizi katika lango la Honduras kunaklo dakika ya 48 ya kipindi cha pili lakini kipa wa Honduras Noel Valladares akababaika na mpira ukavuka laini kisha akaunyofoa mara moja na
kukimbia akitaka kuupiga kama 'goal kick' lakini mpiga kipenga kutoka Brazil Sandro Meira Ricci akapuliza kipenga na kuashiria bao kutokana na mtikiso kwenye saa yake inayoambatana na teknolojia hiyo ya kisasa ya goal line.
Mashabiki na wachezaji wa Honduras waliokuwa ndani ya uwanja wa Porto Alegre walijaribu kupinga kauli ya refarii huyo lakini wapi alihakiki bao hilo la pili usiku huu kwa Ufaransa .
Honduras ilikuwa tayari imempoteza mchezaji wao Palacios mwisho wa kipindi cha kwanza alipoonyeshwa kadi ya pili ya manjano
Teknolojia hiyo inayotumika kwa mara ya kwanza inajumuisha kamera 14 za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa kurekodi picha na sauti kwa kasi mno na mpira ambao inasambaza

Kamera hizo zinauwezo wa kuchukua picha kwa kasi mno (saba kwenye kila lango), katika paa za nyanja zote 12, Brazili.
Kamera hizi zimeunganishwa kwenye tarakilishi inayounda maumbo na kuondoa umbo lolote lile ambalo sio la mpira, kisha kufuata mwenendo wa mpira kwa kadri milimita chache, kampuni hiyo ilisema.
Mpira unapovuka tu mstari wa lango, utakuwa unapeperusha ujumbe kwenye saa yake mwamuzi wa mechi, kisha ujumbe wenye maandishi ‘GOAL’ unatokea kwenye saa hiyo pamoja na mtikisiko (Vibration).
Haya yote yanafanyika kwa muda wa chini ya sekunde moja

Mfumo huo ambao tayari ushajaribiwa na Fifa, katika kombe la Mashirika mwaka uliopita.
Kampuni ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa, ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya michezo.
Hii itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa katika mfumo wa kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High Definition (UHD), ujulikanao kama 4K Format, ambayo kiwango chake ni mara nne zaidi ya kiwango cha
televisheni za kawaida.

Hata ingawa suluhisho hii imetumiwa kwa miaka mingi katika michezo mingine,kama Tennis Cricketi na Raga hii itakua mara ya kwanza teknolojia ya lango la goli kutumika katika kombe la dunia .
Ni mfano mmoja tu wa jinsi kombe hili la dunia litakavyokua lenye teknolojia kubwa zaidi na lenye kujumuisha miundo mbinu ya teknolojia ya karne ya 21.

No comments:

Post a Comment