tuwasiliane

Monday, June 16, 2014

ARGENTINA YAIPIGA BOSNIA 2-1 MESSI ATOA MKOSI

 


Baada mchezo usiyoridhisha katika kipindi cha kwanza, mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi alijifurukuta na kufunga bao la ushindi la Argentina dhidi ya Bosnia-Herzegovina katika mechi yao ya ufunguzi wa kampeini ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil..

Mshambulizi huyo wa timu ya Bracelona ya Uhispania alikuwa na anashtumiwa kwa kutojima anapoichezea timu ya taifa lakini anapoichezea klabu yake anafunga mabao katika takriban kila mechi anayoicheza.
Kwa hivyo Kila aliyekuwa katika uwanja wa kihistoria wa Maracana alikuwa anamtarajia kiungo huyo kuonyesha mbwembwe zake dhidi ya Bosnia inayoshiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza .
Bosnia-Herzegovina, ilikuwa imejifunga yenyewe kunako dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Sead Kolasinac.
Limbukeni hao wa fainali ya kombe la dunia hawakukubali kushindwa bila ya kuonyesha ushindani wao .
Mchezaji wao wa akiba, Vedad Ibisevic, aliipatia timu yake matumaini katika dakika ya 85, alipofunga bao la kwanza la Bosnia, katika kombe la dunia .

Hata hivyo,haikutosha kuwanusuru kibano kutoka kwa Argentina baada ya Messi, kutinga bao lake la kwanza katika fainali hizi za Brazil kunako dakika ya 64.
Argentina inayojivunia vipaji kamilifu katika kila idara ililazimika kumwacha nje mshambulizi wa Napoli, Gonzalo Higuain, akiuguza jeraha.

Izet Hajrovic alikaribia kuisawazishia Bosnia katika dakika ya 13, lakini mlinda lango wa Argentina, Sergio Romero alizuia jaribio hilo la Hajrovic.
Licha ya kuanza kampeni yao vibaya, timu ya Bosnia ilionyesha mchezo mzuri haswa katika safu ya ulinzi ila tu ilihitaji kutia bidii katika mashambulizi yao.

Argentina, Maxi Rodriguez, alipiga mkwaju ambao ulipaa juu ya lango kabla ya muda wa mapumziko.
Jaribio lake Javier Mascherano pia lilizuiwa na mlinda lango wa Bosnia.
Hata hivyo, timu ya Argentina ilishikilia uongozi na kutwaa ushindi.

No comments:

Post a Comment