MIAMBA ya soka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, TP
Mazembe imepigwa kidude kimoja kwa yai dhidi ya El Hilal Omdurani ya
Sudan katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa
barani Afrika.
El Hilal walianza kutibua mipango
ya Mazembe katika dakika ya 51 baada ya Salah Al Jizoli kuandika bao la
kuongoza kufuatia kumalizia pasi nzuri ya Bakri Babeker.
Kipigo hicho cha bao 1-0
kimewafanya Mazembe kuanza vibaya michuano hiyo na sasa watahitaji
kufanya vizuri mchezoz unaofuata, huku wakiwa katika kundi A pamoja na
wapinzani wao wakubwa AS Vita.
Washambuliaji wote wawili wa Tanzania wa TPM walicheza, Mbwana
Samatta akianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda
kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Samatta na Ulimwengu wanatarajiwa
kuondoka asubuhi kuja Dar es Salaam kujiunga na timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Zimbabwe,
kuwania hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco
RATIBA YA MECHI ZA NYINGINE HII HAPA
Saturday 17 May 2014
Esperance (Tunisia) |
v |
ES Setif (Algeria) |
|
20:00 |
|
AS Vita (Congo DR) |
v |
Zamalek (Egypt) |
|
15:30 |
|
CS Sfaxien (Tunisia) |
v |
Al Ahly Benghazi (Libya) |
|
18:00 |
|
Al Ahly Benghazi (Libya) |
v |
Esperance (Tunisia) |
|
18:00 |
|
Zamalek (Egypt) |
v |
Al Hilal (Sudan) |
|
19:30 |
|
TP Mazembe (Congo DR) |
v |
AS Vita (Congo DR) |
|
15:00 |
|
ES Setif (Algeria) |
v |
CS Sfaxien (Tunisia) |
|
19:30 |
|
No comments:
Post a Comment