
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amewasili nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe.
Kazimoto ambaye amewasili nchini
jana (Mei 5 mwaka huu) anatarajia kusafiri leo (Mei 6 mwaka huu) kwenda
Tukuyu mkoani Mbeya ambapo Taifa Stars imeweka kambi yake chini ya Kocha
Mart Nooij kujiandaa kwa mechi hiyo.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager juzi (Mei 4 mwaka huu) ilicheza mechi ya
kirafiki na Malawi (Flames) ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya
kuikabili Zimbabwe (Mighty Warriors). Mechi hiyo dhidi ya Flames
ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na kumalizika kwa suluhu.
No comments:
Post a Comment