
Kaimu kocha wa Manchester United Ryan Giggs amewarai
mashabiki wa klabu hiyo maarufu kuwa wasife moyo ushindi utarejea Old
Trafford katika siku za usoni.
Kigogo huyo wa Manchester United aliwaasa
mashabiki punde baada ya kuingoza Manchester united kuilaza Hull city
mabao 3-1 katika mechi yao ya mwisho ya nyumbani msimu huu wa ligi kuu
ya premia ya Uingereza.Hiyo ndiyo iliyokuwa mechi yake ya mwisho baada ya kushiriki mechi 963 akivalia jezi la Man united.
Kaimu kocha huyo mwnye umri wa miaka 40 alifunga ukurasa wa kipindi chake huko Old Trafford kwa kumkaribisha uwanjani kizazi kijacho cha wachezaji wa timu hiyo alipomkaribisha chipukizi James Wilson.
Tineja huyo alifunga mabao mawili kabla ya Robin van Persie kutamatisha kichapo hicho.
Bao la kufutia machozi la Hull lilifungwa na Matty Fryatt.
Mechi hiyo itakuwa siku ya Jumapili.
Hadi kufikia sasa, kocha Louis van Gaal ndiye anayepigiwa upatu kuchuakua hatamu kama mkuu wa kiufundi Old Trafford ijapokuwa tangazo rasmi linasubiriwa wakati wowote kabla ya mechi dhidi ya Southampton.
No comments:
Post a Comment