MGOGORO
umeibuka kuhusu tarehe ya pambano baina ya bondia bora zaidi duniani,
Floyd Mayweather na Amir Khan kwa sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani
ambalo limepangwa kufanyika Mei mwakani.
Khan
amesema: "Siwezi kuwa tayari kwa tarehe hiyo. Ramadhani haimaliziki
hadi mwishoni mwa Julai na ningependa nipate miezi mitatu ya kuwa
kambini baada ya hapo, kujiandaa na pambano la aina yake. Kurudi mapema
zaidi ulingoni ni mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba na hapo
itabidi nipate mpinzani mwingine.
"Nimemuambia Floyd hayo na amenihakikishia bado nipo kwenye orodha yake,"amesema.
Khan
anapanda ulingoni usiku wa kesho ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini
Las Vegas, Marekani kuzipiga na Luis Collazo, hilo likiwa pambano la
utangulizi kablaya Mayweather kuzipiga na Marcos Maidana.

Mayweather tayari kwa pambano na Marcos Maidana kesho
No comments:
Post a Comment