Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.
Mabadiliko hayo yamepitishwa na
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
iliyokutana jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea
mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya
Mashindano.
Uamuzi huo umefanywa kwa lengo la
kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata
mechi nyingi zaidi za mashindano. Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa
Ligi ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina
mechi 182.
Kuhusu idadi ya wachezaji wa
kigeni kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia uamuzi mapendekezo
katika eneo hilo baada ya kwanza kupata maoni ya klabu za VPL na Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu zitakutana na Rais wa
TFF, Jamal Malinzi.
Mapendekezo ya Kamati ya
Mashindano ni kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee kuwa watano
kama ilivyo katika kanuni za sasa za VPL.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
No comments:
Post a Comment