BEKI
wa klabu ya Leicester City , Jeffery Schlupp ameitwa katika kikosi cha
awali cha wachezai 26 cha timu ya Taifa ya Ghana `Black Stars` kwa ajili
ya kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil.
Schlupp
ameichezea Ghana katika mechi moja tu, lakini kiwango chake cha sasa
kimeisaidia Leicester kupanda ligi kuu nchini England.
Pia
mshambuliaji wa Helsingborg , David Accam ni mchezaji mwingine ambaye
imeshangaza kujumuishwa katika kikosi hicho baada ya kuifungia klabu
yake mabao 10 katika michuano ya ligi ya Sweden.
Kocha wa Ghana, Kwesi Appiah amewaacha baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa akiwemo nahodha John Mensah na Isaac Vorsah.
Michael Essien amechaguliwa kushirikia kombe la dunia kwa mara ya pili
baada ya kukosa la mwaka 2010 kutokana na majeruhi, wakati huo huo
Asamoah Gyan na Sulley Muntari wapo katika mazingira ya kutokea katika
mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya tatu.
The Black Stars wataanza mazoezi mjini Accra mei 20 mwaka huu kabla ya
kusafiri kwenda Amsterdam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Uholanzi
mei 30.
Appiah amesema atapunguza wachezaji mpaka kufikia 23 kabla ya kwenda Marekani kufaya maandalizi ya mwisho huko Miami.
Mechi
ya mwisho ya kirafiki kwa Ghana itakuwa dhidi ya korea kusini mjini
Miami kabla ya kusafiri kwenda Brazil juni 11, siku tano kabla ya mechi
yao ya ufunguzi ya kundi G dhidi ya Marekani.
Pia watachuana na Ujeruani na Ureno katika kundi lao.
KIKOSI CHA GHANA HIKI HAPA
Walinda Mlango: Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars).
Mabeki:
Samuel Inkoom (Platanias), Daniel Opare (Standard Liege), Harrison
Afful (Esperance), Jeffrey Schlupp (Leicester), John Boye (Rennes),
Jonathan Mensah (Evian), Jerry Akaminko (Kisehirspor), Rashid Sumalia
(Mamelodi Sundowns).
Viungo:
Michael Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed
(Kuban Krasnodar), Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu
(Udinese), Afriyie Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert
Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin
Kazan).
Washambuliaji:
Asamoah Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed
Waris (Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux), David Accam (Helsingborg).
No comments:
Post a Comment