tuwasiliane

Tuesday, May 13, 2014

Athari za dawa ya meno kwa mbegu za uzazi

Kemikali zinazopatikana katika baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa kila siku kama vile dawa ya kusugua meno, sabuni na mafuta ya kujikinga kutokana na miale hatari ya jua zinaweza kuharibu mbegu za uzazi za wanaume.
Kwa mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa hizo zina uwezo wa kuanthiri uwezo wa mbegu za uzazi za wanaume kuzalisha mwanamke.

Wanasayansi hao wanasema kwamba bidhaa hizo zina kemikali ambazo zinachangia matatizo ya uzazi kwa wanaume katika nchi za magharibi.
Kemikali zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana kuharibu nguvu za mbegu za kiume kuweza kuzalisha.
Takriban mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa nchini Uingereza anakumbwa na tatizo la kuzalisha na tatizo la utasa ndio kiini kikubwa cha hali hiyo.
Uchunguzi huu ulifanywa na watafiti kutoka Uingereza na Uholanzi na walifanyia uchunguzi kemikali 100 kila siku huku wakigundua kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo ziliathiri uwezo wa Manii kufikia katika mayai ya mwanamke.
Dawa ya meno inaweza kuathiri mbegu za uzazi
Utafiti huu uliandikwa katika jarida la afya la EMBO na watafiti wanasema nyingi ya kemikali hizo hatari zinapatikana katika mafuta yanayotumiwa kujizuia na miale hatari ya jua.
Kemikali nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana katika sabuni na dawa ya kusugua meno.
Uchunguzi wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri uwezo wa Manii ikitafuta mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha.
Kadhalika kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa hisia kwa homoni za mwanamke.
Mabadiliko haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa vigumu kuweza kuzalisha.
Watafiti hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni hatari zaidi kwa mbegu hizo.
Kemikali hizi hujulikana kama kemikali zinazoathiri jinsia kwa sababu ni sehemu ya kemikali zinzzoathiri homoni za mwili wa mwanamume.
Mwaka jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani ya matiti na pumu.
chanzo; BBC SWAHIL

No comments:

Post a Comment