Sherehe za kuhadhimisha miaka 50 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar iliyozaa nchi ya Tanzania zimefanyika leo mjini
Dar es Salaam na kupambwa kwa maonyesho mbali mbali ya kijeshi pamoja na
halaiki zilizoandaliwa na watoto.
Marais wanne wa nchi za Afrika Afrika Mashariki
akiwemo Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre
Nkurunzinza wa Burundi ni miongoni mwa marais waliohudhuria sherehe
hizo.Katika maadhimisho yao pia kulikuwa na maonyesho ya silaha mbali mbali za kivita zikiwemo ndege za kivita pamoja na za kiraia.
Hata hivyo kilichovutia zaidi ni kikosi cha makomandoo wa jeshi la Tanzania ambao walionyesha umahiri wao kupambana na adui bila kutumia silaha na kuvunja vitu vigumu kwa kutumia kichwa pamoja na mikono.
Onyesho jingine lililotia fora ni askari wa miamvuli ambao waliruka kutoka kwenye ndege kwa kutumia miavuli na kutua katika uwanja wa sherehe.
No comments:
Post a Comment