Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
stars imechapwa mabao 3-0 dhidi ya Burundi katika mechi ya kirafiki ya
kuadhimisha miaka 50 ya muungano, uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam.
Mmechi hiyo imechezeshwa na refa Anthony Ogwayo kutoka Kenya
akisaidiwa na Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka
Kenya.
Mwamuzi wa mezani alikuwa Israel Mujuni wa Tanzania wakati Kamishna ni Charles Ndagala.
Mabao ya Burundi yamefungwa na Didier Kavumbagu, Amis Twambwe wanaocheza soka la kulipwa nchini Tanzania.
Bao la tatu la Burundi limefungwa na Yufuf Ndikumana na kuifanya
Stars iwahuzunishe watanzania waliokuwa na furaha ya kuadhimisha miaka
50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment