Young Africans Sports Club
Young
Africans imeanza vizuri mzuguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabo 2-1 dhidi ya timu ya Ashanti
United katika mchezo wa fungua dimba uliofanyika katika dimba la Uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam.
Timu zote zilicheza kwa
kushambuliana kwa zamu lakini mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza
zinamalizika hakuna timu iliyoweza kuliona lango wa timu nyingine
kutokana na washambuliaji wa timu zote mbili kutokua makini katika
umaliziaji.
Dakika ya 51
Young Africans ilipata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake
Didier Kavumbagu ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo
Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Ashanti pamoja na mlinda mlango Daud
Mwasongwe na kupasia Kavumbagu ambaye aliukwamisha mpira wavuni.
Dakika
61 ya mchezo Ashanti United walipata bao la kusawzisha kupitia kwa
mshambuliaji Bright Obinna aliyemalizia krosi ya mshambuliaji Hussein
Sued aliyemtoka mlinzi wa kulia wa Young Africans na kupiga krosi hiyo
iliyomkuta mfungaji Obinna.
David Luhende aliipatia Young Africans
bao la pili la na la ushindi dakika ya 80 ya mchezo baada ya kuwatoka
walinzi wa Ashanti mpaka ndani ya eneo la hatari na kuachia shuti kali
ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Ashanti United na kujaa wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 1 Ashanti United.
Mara
baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der
Pluijm alisema kikubwa anashukuru timu yake imepata pointi tatu, lakini
kimchezo haikucheza vizuri hiyo inatokana na uchovu wa safari na
mabadiliko ya hali ya hewa na kusema mchezo unaofuata vijana wake
watakuwa vizuri tayari.
"Ukitazama jinsi walivyokuwa wakicheza
katika mechi za nchini Uturuki na walivyocheza ni tofauti, siwezi
kuwalaumu lakini kikubwa natambua wamechoka, wana uchovu wa safari kwani
wamepumzika masaa 15 tu kabla ya mchezo na hali ya hewa waliyotoka ni
baridi na hapa ni joto hivyo naamini baada ya siku chache watakuwa
wamerejea katika hali zao za kawaida" alisema Hans.
Young Africans: 1.Dida, 2.Juma, 3.Oscar, 4.Twit, 5.Yondani, 6.Domayo, 7.Ngasa, 8.Niyonzima, 9.Kavumbagu/Javu, 10.Bahanuzi/Msuva, 11.Luhende
No comments:
Post a Comment