tuwasiliane

Sunday, January 26, 2014

Chelsea yamsajili Mohamed Salah

 
Chelsea imemsajili mcheza kiungo wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, kutoka kwa Basel ya Uswisi kwa kitita cha pauni milioni kumi na moja.

Salah mwenye umri wa miaka 21, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na pia kujadiliana kuhusu mshahara wake kabla ya kuhamia uwanja wa Stamford Bridge.

Mahasimu wa Chelsea katika ligi kuu ya Premier, Liverpool walikuwa wameanzisha mazungumzo na klabu hiyo ya Basel, kutaka kumsajili mchezaji huyo.

Siku ya Jumatano, Chelsea ilikubali kumuuza Juan Mata, kwa Kalbu ya Manchester United.
Ripoti zinasema, usajili wa Mata uliogharimu United pauni milioni 37, uliimarisha nafasi ya Chelsea ya kumnunua Salah ambaye atakuwa mchezaji wao wa tatu, kusajiliwa mwezi huu baada ya Nemanja Matic na Betrand Traore.

Kusajiliwa kwake sasa kutampa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, nafasi zaidi ya mashambulizi baada ya De Bruyne kusajiliwa na klabu ya Wolfburg kwa mkopo.
Salah ambaye anaweza kucheza katika nafasi tofauti za mashambulizi, amekuwa akitafutwa na vilabu kadhaa, baada ya kuonyesha mchezo safi wakati wa mechi zao za ligi ya Uropa msimu uliopita na pia michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu huu

No comments:

Post a Comment