SIMBA
SC wamefuzu kuingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya usiku huu
kuilaza mabao 2-0 URA ya Uganda kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Shujaa
wa Simba SC leo alikuwa ni kiungo mwenye kipaji, Amri Ramadhani Kiemba
aliyesababisha bao la kwanza na kufunga mwenyewe la pili.
URA
ilipata pigo mapema dakika ya 32 baada ya mshambuliaji wake hatari,
Owen Kasuule kutolewa nje kwa nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea
rafu winga msumbufu wa Simba SC, Ramadhani Singano ‘Messi’
Dakika
45 za kipindi cha kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na
kipindi cha pili ndipo Simba SC inayofundishwa na Mcroatia, Zdravko
Logarusic ilipofungua makucha yake.
Kona
maridadi ya Kiemba ilimkuta beki Donald Mosoti, aliyemsetia beki pacha
wake wa kati, Joseph Owino akafunga bao la kwanza dakika ya 49.
Wakati
URA wanahaha kusaka bao la kusawazisha, Simba SC walifanya shambulizi
zuri na krosi maridadi ya Haroun Chanongo ikaunganishwa nyavuni na Amri
Kiemba dakika ya 52 kuipatia Simba SC bao la pili.
Bao hilo liliinyong’onyesha kabisa URA, ingawa iliendelea kupambana kupata japo bao la kufutia machozi.
Kwa
ujumla, URA iliathiriwa mno na kutolewa na mshambuliaji wake hatari,
Owen Kasuule, kwani ndiye tegemeo lake la mabao kwa pamoja na Feni Ali.
Baada ya mechi, Kiemba alipewa king’amuzi cha Azam TV kwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Simba SC sasa itapambana na KCC ya Uganda pia katika Fainali Jumatatu Saa 10:00 Uwanja wa Amaan.
Ikumbukwe Simba na KCC zote zimetokea Kundi B na katika mechi baina yao, zilitoka sare ya bila kufungana.
Kikosi
cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid
‘Baba Ubaya’/William Lucian 'Gallas', Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas
Mkude, Haroun Chanongo, Amri Kiemba/Said Ndemla, Ramadhani Singano
‘Messi’, Amisi Tambwe/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Awadh Juma/Uhuru
Suleiman.
URA;
Mugabi Yassin, Samuel Ssenkoom, Alan Munamba/James Kasibante, Mussa
Doca, Jonathan Mugabi, Oscar Agaba, Augustine Nsumba, Owen Kasuule,
Erisa Sekisambu/Ngama Emmanuel, Feni Ali/Milos Ilic na Hashimu Sempalia.
No comments:
Post a Comment